Saturday, May 23, 2015

UWANJA MKUBWA ZAIDI DUNIANI


Rungrado Stadium , Pyongyang, Korea Kaskazini huu ndiyo uwanja mkubwa michezo duniani. Hutumika kwa michezo mbali mbali ikiwemo kandanda.

Ndiyo uwanja mkubwa zaidi duniani ambao hautumiwi kwa mbio za magari.
Una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 150, 000. Ndiyo hutumiwa na timu ya Taifa ya Korea ya Kaskazini....


Duru zisizokuwa za soka zinadai kwamba ni katika uwanja huu ambapo majenerali kadhaa waliuawa kwa kuchomwa moto wakiwa hai baada ya kuhusishwa na jaribio la mapinduzi la kutaka kumuua kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-il

Credit to: Baraka Mbolembole
Gosbert Massawe

Thursday, May 21, 2015

Uoga wa Raia wa Kitanzania Wakwamisha Mambo


Yako mambo mengi madogo madogo ambayo watu hutenda na kuleta mabadiliko. Lakini, kila wakati lazima pawepo msukumo ili kufanikiwa, iwe katika nyanja za elimu, afya bora, mazingira safi na mengineyo.
Hali ya mazingira wakati huu ina umuhimu zaidi kuliko ilivyokuwa siku za nyuma kutokana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na athari zake zisizofikirika katika maendeleo ya binadamu.
Wakati wanasayansi wanajadili uhusiano kati ya uunguzaji wa mafuta ya asilimwamba, kuongezeka kwa hewa ukaa na kupanda kwa halijoto duniani, Watanzania wanahitajika kuchukua hatua za haraka kurekebisha uharibifu mkubwa wa mazingira yao.
Ni zaidi ya miongo miwili tangu mfumo wa siasa za vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, lakini raia wa nchi hii bado si wepesi kuanzisha au kujiunga na vikundi vya hiari ambavyo vinaweza kuharakisha maendeleo na kuepusha mgogoro wa kimazingira ambao unaweza kutokea.
Shauku iliyoambatana na ushindi wa jumuiya za kiraia katika kuanzisha vyama vya siasa imefifia. Hata baadhi ya vyama vimepotea hivyo hivyo.
Lakini bado watu wanalalamika kuhusu ongezeko la umasikini; elimu duni; uhaba wa huduma bora za afya; unyanyasaji wa wanawake na watoto; ubaguzi wa kijinsia katika taratibu za kufanya maamuzi; ukosefu wa makazi bora; hali duni ya huduma za usafi wa mazingira na mambo mengine mengi katika mlolongo wa mapungufu katika maisha ya kila siku Tanzania.
Wakulima wadogo hawana imani tena na vyama vya ushirika. Katika mikoa ambapo vyama hivyo vilikuwa mhimili wa maendeleo kutokana na uuzaji wa mazao ya biashara hali imerudi nyuma baada ya kushuka kwa bei za mazao pamoja na uzalishaji.
Hali ni hiyo hiyo mijini ambako vyama vya ushirika wa walaji vilikuwa vimestawi kutokana na mafanikio ya kutetea haki za walaji na kuwasogezea bidhaa karibu. Wakati walaji wakiongezeka kila mwaka, vyama hivyo vimetoweka.
Mvua kubwa ziliponyesha wiki ya kwanza ya mwezi huu wa Mei katika ukanda wa pwani na kusababisha uharibifu uliotokana na mafuriko Dar es Salaam na Zanzibar, watu wengi walianza kutafakari wakijiuliza ni kitu gani kimevuruga mwenendo wa maisha. Zama zimepita ambapo jumuia zilijitoa kukabili changamoto kama hizo kabla ya kuomba msaada kutoka nje.
Kwa kiwango kikubwa mafuriko ya sasa ni changamoto kwa serikali kufanya matengenezo, kupanga na kujenga miundombinu inayofaa.
Maafisa wa serikali wamewaambia wakazi wa mabondeni ambayo hufurika wakati wa mvua wajijue wenyewe, kwa sababu mara kwa mara wamekaidi kufuata ushauri wa kuhamia sehemu za miinuko. Lakini waathirika pamoja na familia zao wanalia wapate msaada ambao haupatikani.
Wiki moja kabla ya mafuriko, wakazi wa mitaa ya Avocado, Kawe Beach and Mzimuni wilayani Kinondoni katika jiji la Dar es Salaam walitangazwa katika taarifa za televisheni kuwa ni mfano wa watu wanaojali kupendezesha mazingira yao.
Wana nia thabiti kutunza usafi wa mitaa, siyo tu kwa kuondoa taka lakini pia kuzuia madawa ya kulevya na uhalifu, vitu ambavyo vimeharibu sifa za maeneo mengi ya mijini na kuwanyima wananchi raha ya kujisikia kuwa na jumuiya zao wenyewe.
Wakati huo, mbunge wa jimbo la Ludewa kusini mwa Tanzania amefaulu kuwaunganisha wananchi, bila kujali vyama vyao vya siasa, wafanye kazi bila malipo kukamilisha mradi wa usambazaji umeme vijijini. Kwa kuwashawishi, ameweza kuwaongoza wafanye kazi ambayo italeta mabadiliko ya kudumu katika maisha baada ya vijiji vyao kupata umeme kutoka gridi ya taifa.
Hivyo basi kwa nini vikundi vya kiraia vilivyokuwa na mwamko zamani vimefifia baada ya demokrasia kuimarishwa? Kila mtu angetarajia kuona mwamko wa kiraia umeshamiri badala ya kufifia katika mfumo mpya wa kidemokrasia.
Kwa bahati mbaya, sivyo ilivyo. Jumuia nyingi zinakosa viongozi wa kuwashikia mwenge na kuwahamasisha ili watende mambo ambayo yataiwezesha nchi hii iwe mahali bora pa kuishi.
Mwandishi: Anaclet Rweyagura/ DW Dar es Salaam
Mhariri: Daniel Gakuba
Gosbert Massawe

Mgombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia Kajiondoa

Mgombea wa kiti cha Urais wa Fifa Michael van Praag amejiondoa kwenye kinyang'anyiro.
Kujiondoa kwa mwenyekiti huyo wa shirikisho la kandanda la Uholanzi sasa kumewaacha wagombea wawili pekee wanaowania kiti hicho na rais wa FIFA Sepp Blatter.
Van Praag, mwenye umri wa miaka 67, amesema atamuunga mkono Prince Ali Bin Al-Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 29 Mei.

Mchezaji wa zamani wa kiungo kutoka Ureno Luis Figo, mwenye umri wa miaka 42,ni mgombea mwingine katika uchaguzi huo.
Blatter,mwenye umri wa miaka 79, anatarajiwa kushinda muhula wake wa tano akiongoza soka duniani. FIFA ina wanachama 209 na kila mmoja ana kura moja.
Vyama vingi vya soka vilionyesha nia ya kumuunga mkono Prince Ali.
Hata hivyo chama cha soka cha Uskochi awali kilikuwa kimesema kitamuunga mkono Van Praag.
Kujiuzulu kwake kumekuja baada ya mgombea mwingine,katibu mkuu wa zamani wa FIFA, mfaransa Jerome Champagne kujiondoa mwezi Februari.
"van Praag anasema kuwa atamuunga mkono Al -Hussein"
Uchaguzi huo utafanyika mjini Zurich katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa FIFA.
Mshindi lazima apate theluthi mbili ya kura zote zilizopigwa katika awamu ya kwanza.

Credit to: bbcswahili
Gosbert Massawe

Monday, May 18, 2015

Kukoroma Noma sana Usingizini






Gosbert Massawe

Video: kituko cha Simu.


Gosbert Massawe

New Song: Rap Wity Melody - Chidy Mentary







Gosbert Massawe